Wednesday, July 10, 2013
Umeskia hii: Chid Benz Na Ney washrikishwa Kwenye Track moja bila wao wenyewe Kujua? Wimbo wenyewe huu hapa sasa!!!
Hivi karibuni msanii Baghdad alitoa ngoma yake mpya akishirikiana na wasanii wawili ambao inasemekana kwamba hawana mahusiano mazuri. Wasanii hao ni Chidy Benz na Ney wa Mitego, kwa pamoja walishiriki kwenye ngoma moja ya Baghdad bila kujua kama wapo kwenye ngoma moja. Baadaye kutokana na ratiba zao tofauti wakafanya video siku tofauti na katika location tofauti lakini kwa ajili ya ngoma moja hiyohiyo. Baghdad baada ya kuachia audio yake ambayo ilipata attention baada ya kusikika kwamba Ney wa Mitego na Chidy Benz wapo kwenye ngoma moja.
Habari kutoka kwenye chanzo cha uhakika zinasema kwamba Chidy Benz kutokana na kutokuwa na taarifa juu ya collabo hiyo, amepiga stop kutoka kwa video yake. Source ya story hii inaendelea kuhabarisha kwamba kuna mazungumzo yanafanyika na Chidy Benz kupata njia nzuri ya kuitoa video hiyo baada ya kuweka mambo kadhaa sawa kwenye maongezi hayo..
Track yenyewe ndio hii:
Tuesday, July 9, 2013
VIDEOS: CHEKI PAMBANO LA NGUMI HALIMA MDEE VS WOLPER!!
KUCHEKI VIDEOS ZA PAMBANO LA NGUMI KATI YA HALIMA MDEE DHIDI YA JACKLINE WOLPER KWENYE TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI, >>CLICK HAPA<<
STAR WA VIDEOS (AGNESS MASOGANGE) AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI!!!
Mwanadada Agnes Gerald (Agnes Masogange) ambaye amejipatia umaarufu kwa kushiriki kwenye video za mastaa mbalimbali wa muziki hapa Tanzania, ni mmoja kati ya Wanawake wawili raia wa Tanzania waliotambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Ripoti ya awali kutoka Afrika Kusini inasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Monday, July 8, 2013
BARCELONA REACHED AN AGREEMENT WITH ATLETICO MADRID OVER THE TRANSFER OF DAVID VILLA!!!!
Barcelona have confirmed they have reached an agreement with Atletico Madrid over the transfer of forward David Villa.
Subject to the agreement of personal terms and passing of a medical, the Spain international will move to the Vicente Calderon in a deal worth an estimated maximum of.... >>Read More<<
Saturday, July 6, 2013
SAD: Mtanzania auawa nchini Marekani
POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku.Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili.
Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.
“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC
alipohojiwa na News4.
alipohojiwa na News4.
Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa.
“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.
Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana.
Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.”
Friday, July 5, 2013
SA: Mahakama yasababisha Ufa na Uhasama kwa familia ya Mandela!!!
Vita ya wapi atakapozikwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela imefikia tamati na sasa ni rasmi kwamba atazikwa Qunu uamuzi ambao umeacha ufa na uhasama mkubwa katika familia ya kiongozi huyo.
Jana, mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela ambao ni marehemu ilitarajiwa kuzikwa upya katika eneo la Qunu, yakiwa ni mazishi ya mara ya tatu tangu walipofariki dunia katika vipindi tofauti, ukiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Eastern Cape.
Thursday, July 4, 2013
Makachero wayafichua mapya mabomu Arusha
TAARIFA za awali kutoka kwa makachero wa Jeshi la Polisi nchini zimefanikiwa kubaini mtandao wa ulipuaji mabomu katika jiji la Arusha, imefahamika. Mpaka sasa taarifa zinadai mtandao uliohusika na milipuko miwili iliyotokea kwa nyakati tofauti jijini hapa ulipangwa ndani ya... >>Read More>>
Subscribe to:
Posts (Atom)







































