Blogger Widgets

Monday, May 19, 2014

HII NAYO KALI,, CHEKI RAISI HUYU WA NCHI ANAYECHEZA SOCCER LA KULIPWA..!!!


Nikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wan chi kwenye hili soka unaweza kuotea ni namba ngapi?tunaweka kwenye story kubwa kutokana na kutotokea mara kwa mara kwa taarifa hizi.
prezzzSasa unaambiwa Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo wa kati kuanzia Agosti mwaka huu na mgongoni atakua na jezi namba 10.
Mshahara wa Rais Morales kwenye timu hii atakua akilipwa dola $213 kwa mwezi ambapo ni zaidi ya laki 3 kwa pesa za Kitanzania ,klabu hiyo ipo Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.
prezKwa sasa Mashabiki wanamsubiri president huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki mzuri wa michezo kucheza mpira.ataichezea Sports Boys, timu iliyopo kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.
Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema kuwa rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mchuano watakaokuwa wanacheza,hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.
Kumbukumbu inaonyesha mwaka wa 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.
Ingawa Mwaka wa 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa.