Blogger Widgets

Saturday, May 24, 2014

Je, Hiki anachofanya Tony Braxton kwa watoto wake ni sahihi??

"Twist Of Faith" - Los Angeles Premiere
Katika harakati za kutafuta mbinu bora za malezi mazuri kwa watoto wake, Nyota wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Tony Braxton anafanya jitihada za kuwafundisha watoto wake usimamizi mzuri wa fedha kwa kuwalipisha kodi ya kuishi katika nyumba yake kwa madai kuwa anawafundisha maisha.
Braxton aliyewahi kutamba na vibao vikali kama Unbreak My Heart ni mama wa watoto wawili wa kiume Denim mwenye umri wa miaka 12 na Diezel mwenye miaka 11. Ingawa mafanikio yake makubwa kama mwanamuziki yamesaidia kulea familia na kutoa mahitaji muhimu ya familia yake, Tony ameanza utaratibu huo kwa watoto wake ili wajue thamani ya dola.
Katika mahojiano na kipindi cha Televisheni cha Queen Latifah nchini Marekani, Braxton ameweka wazi kuwa watoto wake wanapata dola 10 na 12 kwa wiki ambapo mmoja humlipa dola mbili na mwingine tatu ambapo wanatakiwa pia kulipia senti 75 kwa ajili ya gesi na umeme.
Wakati wazazi wengine wakiwa hawafanyi kitendo hicho, Kwa upande wake Braxton anasisitiza kuwa ana matumaini kuwa mafunzo hayo ya matumizi mazuri ya pesa kwa watoto wake yanawaandaa vyema katika maisha yao ya baadae.
Braxton amefafanua kuwa kwa kufanya watoto wake watajua thamani ya fedha na watakapokuwa wakubwa watahitajika kulipa bili zote kwa wakati kwa kuwa wamezoea utaratibu huo.