Thursday, July 4, 2013
Tuesday, July 2, 2013
Mhe. Rais Obama atembelea Mitambo ya Symbion na kuzindua mpango wa maendeleo ya nishati Afrika
| Wageni mbalimbali wakiwemo Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini wakimsikiliza Mhe. Rais Obama |
![]() |
| Mheshimiwa akionesha umahiri wake kwenye ball control kwa kutumia kiffa hicho chenye mfano wa mpira wa miguu!! |
| Mhe. Rais Obama na Mhe.Kikwete wakijaribu kupigiana kifaa hicho mfano wa mpira. |
| Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakiangalia kifaa hicho kikiunganishwa kwenye moja ya taa kabla ya kuwashwa. |
Monday, July 1, 2013
UPDATES: Je wajua Rais mstaafu wa Marekani, George W. Bush naye yupo Tanzania??
Rais Barack Obama amewasili jijini Dar es Salaam mapema leo kuhitimisha ziara yake barani Afrika na wakati akiwa hapa anatarajiwa kukaribishwa na sura anayoifahamu.
Rais aliyemtangulia, George W. Bush pia atakuwa hapa nchini kuhutubia mkutano wa Wanawake wa Afrika, na marais hao wawili wamepanga kukutana kwenye Ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam kesho.
Obama na Bush wataweka mashada ya maua kukumbukia mlipuko wa bomu kwenye ubalozi huo ambao uliua watu 11 mwaka 1998.
Rais huyo wa sasa alikwenda Afrika Kusini baada ya kwanza kutembelea Senegal katika safari ya kuimarisha mshikamano wa demokrasia kati ya Marekani na Afrika.
Amepanga kukutana na Rais Jakaya Kikwete, na pia wafanyabiashara kadhaa wa Marekani na Afrika kwa matumaini ya kuimarisha biashara katika bara hilo.
Kesho asubuhi atakutana na Bush kwenye ubalozi huo kabla ya kuhutubia kuhusu nishati ya umeme barani Afrika, na kisha ataondoka kurejea Washington.
Kwa upande wake, Bush anahudhuria mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya George W. Bush.
Wake na marais hao wawili, Michelle Obama na Laura Bush, watajumuika kwenye mkutano huo kwa majadiliano kuhusu kusaidia elimu kwa wanawake, afya na ajira.
Bush amejikita zaidi kwenye kazi yake ya kujitolea kuhusu Afrika tangu aachie madaraka ya urais, na anakumbukwa mno katika bara hili kwa kazi yake wakati alipokuwa Rais.
Reported by >>> Walee
OBAMA AWASILI TANZANIA!!!
![]() |
| Barabara za jiji zikisafishwa kwa ajili a kiongozi huyo mkubwa!! |
![]() |
| Eneo la Ikulu likiwa limeandaliwa tayari kwa mapokezi! |
![]() |
| Eneo ambalo Rais Obama na Mwenyeji wake watazungumza na waandishi wa Habari!! |
![]() |
| Air Force one, Ndege maalum kwa Rais wa Marekani! |
![]() |
| Rais kikwete akisalimiana na Wananchi waliopo eneo la ikulu kwa ajili ya Mapokezi ya Obama |
![]() |
| Watu wliokusanyika kushuhudia Ujio wa Obama jijini Dar es salaam! |
![]() |
| Rais Obama akijaribu kucheza ngoma zilizokuwa zikitumbuiza wakati wa Mapokezi |
ALL PHOTOS BY: CHINDO MKAZUZU
Stay with us for more Photos and Updates!!
Subscribe to:
Posts (Atom)





















