Friday, June 21, 2013
Thursday, June 20, 2013
Hali ilivyokuwa leo Mjini Arusha!!!!
Maandamano Makubwa ya wafuasi wa CHADEMA wakielekea kuaga miili ya waliopoteza Maisha katika mlipuko wa Bomu, jumamosi iliyopita!!
Hivi ndivyo hali ya mji ilivyokuwa leo..
Hivi ndivyo hali ya mji ilivyokuwa leo..
Wednesday, June 19, 2013
Tuesday, June 18, 2013
Hali si shwari tena Arusha! Mabomu ya machozi Yatawala!!!!
Kwa habari tulizozipata hivi punde ni kwamba, mabomu ya machozi yanarindima mjini Arusha kuwatuliza wafuasi wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo waliokuwa wamekusnyika tena viwanja vya Sowetho kufuatia tukio lililotokea Juzi jumamosi. la kulipuliwa bomu katika mkutano wa kampeni.
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo >> SOMA ZAIDI>>
Kombe la Mabara, Brazil!!
Italy na Spain zote zaibuka na ushindi katika match zilizochezwa jana katika viwanja tofauti!!
PATA HABARI ZAID, MATOKEO, NA PICHA YA MATCH HIZO HAPA>>
PATA HABARI ZAID, MATOKEO, NA PICHA YA MATCH HIZO HAPA>>
Monday, June 17, 2013
KAULI YA RAIS KUTOKANA NA MLIPUKO ULIOTOKEA ARUSHA!!
MLIPUKO wa bomu uliotokea Arusha na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 70 limezua utata kutokana na hisia tofauti za viongozi mbalimbali nchini waliozungumzia suala hilo, huku Rais Jakaya Kikwete akisema haamini kama Watanzania sasa wamefikia hatua ya kuanza kuhasimiana kwa misingi ya kisiasa.
Hii ni mara ya pili kwa Jiji la Arusha kushambuliwa kwa bomu baada ya lile lililorushwa kwenye Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi kwenye Parokia ya Olasiti wakati wa sherehe ya uzinduzi wake Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu na kujeruhi 64. Wakati Rais Kikwete akisema hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wamesema tukio hilo ni la kisiasa na lilipangwa.
Kufuatia tukio hilo, uchaguzi wa kata nne za Arusha mjini umeahirishwa hadi Juni 30.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana imeeleza kuwa Rais Kikwete ambaye yuko nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa nchi zilivyoendelea kiviwanda(G8), alisema haamini kama Watanzania ama wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kudiriki kufanya matukio ambayo yanahatarisha usalama wa watu.
“Mimi siamini kuwa Watanzania au wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kufanyiana matendo ya unyama wa aina hii. Naamini kuwa hiki ni kitendo cha mtu ama watu wasioitakia mema nchi yetu, watu ambao wanatafuta kila sababu ya kupandikiza chuki miongoni mwa raia ama makundi ya raia, ili nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa.”
Sunday, June 16, 2013
Habari zaidi tukio la Mlipuko Arusha!!
Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.
Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.
Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.
Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.
Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.
Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani.
Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.
Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki.
Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo. Source: MWANANCHI
Saturday, June 15, 2013
BREAKING NEWS!!! BOMU LAKUTEGWA LALIPUKA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MADIWANI ARUSHA.
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba, kumetokea mlipuko wa bomu linalosadikiwa ni la kutegwa, katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kampeni za udiwani Arusha, maeneo ya viwanja vya Soweto, kaloleni Arusha. Mpaka sasa habari zilizotufikia ni kwamba watu wawili wamepoteza maisha, na majeruhi wanakimbizwa hospitali ya mkoa MT.Meru.
Mkutano huo ndio ulikuwa wa mwisho kabla ya uchaguzi wa madiwani hapo kesho. Mh. Freeman Mbowe nae alikuwa moja ya watu waliohudhuria mkutano huo. Habari zaidi zitakujia kutoka hapa!
Subscribe to:
Posts (Atom)














































