Mkude Simba ni mmoja tu ukimuona mwingine ujue feki maana WATANZANIA wanapendaga sana kutafuniwa utasikia kama sio msanii mwenzangu litatokea lijitu tu.!! ila Mungu ni mmoja na yu pamoja nami wakati wa Kitale Anakuja walitokea kina KITALE wengi..!!
Saturday, May 31, 2014
KATIKA PICHA NI GEORGE TYSON MASAA MANNE KABLA YA AJALI ILIYOCHUKUA UHAI WAKE NA GARI ALILOPATA NALO AJALI!!

Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
SOURCE>> dJChoka
Tuesday, May 27, 2014
WACHEZAJI NA KOCHA, WOTE NDANI YA STUDIO! HUU NDIO WIMBO WALIOIMBA WACHEZAJI WA MADRID BAADA YA KUSHINDA UEFA!!
Inaskitisha hii! Meneja Wa MJ alipanga kumteka staa huyoo..!!!
Meneja wa aliyekuwa mfalme wa Pop duniani Michel Jackson alijaribu kumteka staa huyo kumuokoa kutokana na dawa za kulevya.
Meneja huyo Ron Weisner ambaye ndiye aliyekuwa akidhibiti taaluma na kipaji cha marehemu Michael tangu enzi za ujana wake alikuja na.... >>READ MORE<<
Saturday, May 24, 2014
Je, Hiki anachofanya Tony Braxton kwa watoto wake ni sahihi??
Katika harakati za kutafuta mbinu bora za malezi mazuri kwa watoto wake, Nyota wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Tony Braxton anafanya jitihada za kuwafundisha watoto wake usimamizi mzuri wa fedha kwa kuwalipisha kodi ya kuishi katika nyumba yake kwa madai kuwa anawafundisha maisha.
Braxton aliyewahi kutamba na vibao vikali kama Unbreak My Heart ni mama wa watoto wawili wa kiume Denim mwenye umri wa miaka 12 na Diezel mwenye miaka 11. Ingawa mafanikio yake makubwa kama mwanamuziki yamesaidia kulea familia na kutoa mahitaji muhimu ya familia yake, Tony ameanza utaratibu huo kwa watoto wake ili wajue thamani ya dola.
Katika mahojiano na kipindi cha Televisheni cha Queen Latifah nchini Marekani, Braxton ameweka wazi kuwa watoto wake wanapata dola 10 na 12 kwa wiki ambapo mmoja humlipa dola mbili na mwingine tatu ambapo wanatakiwa pia kulipia senti 75 kwa ajili ya gesi na umeme.
Wakati wazazi wengine wakiwa hawafanyi kitendo hicho, Kwa upande wake Braxton anasisitiza kuwa ana matumaini kuwa mafunzo hayo ya matumizi mazuri ya pesa kwa watoto wake yanawaandaa vyema katika maisha yao ya baadae.
Braxton amefafanua kuwa kwa kufanya watoto wake watajua thamani ya fedha na watakapokuwa wakubwa watahitajika kulipa bili zote kwa wakati kwa kuwa wamezoea utaratibu huo.
Tuesday, May 20, 2014
ULIKUWA UNAJUA?? HUYU NDIO RAIS MASKINI ZAID DUNIANI..!!!

Rais Jose Mujica akiwa na Papa Francis
Sifa kwa wanasiasa kokote duniani ni nadra, hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu wamemmiminia sifa Rais wa Uruguay baadhi wakitamani kama marais wao wangekuwa kama Rais Jose Mujica wa Uruguay.
Kwenye Twitter kuna zaidi ya ujumbe laki moja wa watu nchini Uhispania wakitamani kama...
Monday, May 19, 2014
HII NAYO KALI,, CHEKI RAISI HUYU WA NCHI ANAYECHEZA SOCCER LA KULIPWA..!!!
Nikikupa nafasi ya kuniambia namba ngapi atakua anacheza huyu president wan chi kwenye hili soka unaweza kuotea ni namba ngapi?tunaweka kwenye story kubwa kutokana na kutotokea mara kwa mara kwa taarifa hizi.

Mshahara wa Rais Morales kwenye timu hii atakua akilipwa dola $213 kwa mwezi ambapo ni zaidi ya laki 3 kwa pesa za Kitanzania ,klabu hiyo ipo Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.

Timu hiyo ambayo ipo katika ligi ndogo imesema kuwa rais huyo atakuwa akicheza kwa dakika 20 katika kila mchuano watakaokuwa wanacheza,hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.
Kumbukumbu inaonyesha mwaka wa 2007 rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.
Ingawa Mwaka wa 2006 alipata matatizo uwanjani kwa kuvunjika mguu wakati alipogongana na kipa.
Sunday, May 18, 2014
Friday, May 16, 2014
Thursday, May 15, 2014
Wednesday, May 14, 2014
UMESIKIA HII?? DIAMOND PLATNUMZ AZIDI KULA SHAVU,, Sasa amekuwa nominated kwenye tuzo za BET..!!
Baada ya msanii mkubwa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz kuweka headlines mitaani kwa kushiriki kwenye tuzo za MTV base (Mama Awards), Amepata tena dili hili kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa wasanii wa bongo. Sasa Diamond Platnumz ametajwa kuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za kituo kikubwa cha television cha marekani maarufu kama BET (Black Entertainment Television) ambapo yupo katika kipengele cha wanaogombea tuzo ya BEST INTERNATIONAL ACT AFRICA. Wasanii wengine katika kipengele hicho ni pamoja na Davido wa Nigeria, Mafikizolo, kundi toka Afrika kusini, Tiwa Savage wa Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana..
Katika kusibitisha hilo, BET kupitia page yao ya twitter walisibitisha kwa kumpongeza diamond kwa ujumbe mfupi..

Aljerry'12 inampongeza Diamond kwa dili kubwa hiyo.. Now go make Tanzania Proud...!!!!
Tuesday, May 13, 2014
Monday, May 12, 2014
Saturday, May 10, 2014
Thursday, May 8, 2014
WAGONJWA WA DENGUE WAFIKIA 376...!!

Homa ya dengue inaendelea kushika kasi nchini baada ya takwimu za Januari hadi juzi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kuonyesha kuwa watu 376 wamekwishagundulika kuugua ugonjwa huo.
Mtaalamu wa Ufuatiliaji wa Magonjwa wa wizara hiyo, Dk Janeth Mugamba alisema..... >>Soma Zaidi<<
Wednesday, May 7, 2014
Tuesday, May 6, 2014
Hello Hello Tanzania..!! Ulikuwa unajua wimbo huu ni kazi ya Ditto na Amini? Sikiliza na download hapa..!!
Ni wimbo uliotungwa na Amini pamoja na Ditto wa THT ambao umekua maarufu kwa kipindi kifupi cha sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar...
Sunday, May 4, 2014
Hawa ndio washindi wote wa Tuzo za KTMA!! Diamond Platnumz, kaondoka na tuzo zote saba katika Categories zote Saba alizokuwa Nominated!!
Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul "Diamond Platinumz" Usiku wa Jana May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).
Diamond amejinyakulia tuzo zifuatazo:-
Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.
Washindi wengine katika tuzo hizo ni hawa wafuatao:
Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili vya
Tanzania- Bora Mchawi - Dar Bongo
Massive.
Msanii Bora Chipukizi - Young Killer.
Wimbo Bora wa Zouk kwa 2014
- Yahya by Lady Jaydee.
Wimbo Bora wa Afro Pop - Number One by Diamond Platinumz.
Baadhi ya Picha ya mambo yaliyojiri kwenye tuzo za KTMA,, Diamond na Wema Waendelea Ku-make Headlines..!!!!
Diamond Na Wema Sepetu on Stage baada ya kuitwa kupokea Tuzo..!!
Weusi hatuna Kwereee!!!!! kundi la Weusi on stage wakifanya yao!!
>>SOMA ZAIDI<<
Subscribe to:
Posts (Atom)